UINGEREZA YASTISHA MISAADA RWANDA
Uingereza yasitisha misaada Rwanda
Uingereza imetangaza kusitisha misaada kwa nchi ya Rwanda.
Taarifa
iliyotolewa na Serikali ya Uingereza leo, imebainisha kuwa Rwanda
inahusika kwa namna moja au nyingine katika mgogoro wa kivita nchini
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Serikali
ya Uingereza imesema kuwa nchi yake haiwezi kuipa msaada Rwanda wakati
yenyewe inahusika na matatizo ya kivita nchini DRC.
Imeeleza
kuwa misaada ambayo ilikuwa itolewe hivi karibuni na Serikali ya
Uingereza kwenda Rwanda, imesitishwa na haitatoka mingine kwa kipindi
hiki.
Imezidi
kubainisha kwamba endapo Rwanda itajirekebisha na kuacha kuwasaidia
waasi, basi Uingereza itafikiria kurudisha misaada kwa nchi hiyo.
Uingereza
imesisitiza kwamba imeamua kuinyima msaada Rwanda baada ya kupatikana
kwa ushahidi usio na shaka kwamba nchi hiyo inakiwezesha Kikundi cha M23
ambacho kinaundwa na Kabila la Banyamulenge walioamua kuasi dhidi ya
Serikali ya DRC.
Kabila la Banyamulenge linaundwa na Wakongo wenye asili ya Rwanda.
BY DEIWAKA
Post a Comment