Header Ads

test

HABARI KAMILI KUHUSIANA NA MLIPUKO WA BOMU ARUSHA..

Leo asubuhi jiji la arusha lilipata mshtuko mkubwa na simanzi nzito baada ya kutokea kwamlipuko wa mabomu uliotokea katika kanisa la kikatoliki huko olasisti nakupelekea vifo na majeruhi kwa baadhi ya waumini waliohudhuria katika sherehe ya ufunhuzi wa kanisa.. 
CHANZO..
Haya nimaelezo ya kijana aliyedai kuwa alishuhudia tukio hilo.
Kijana huyo(chini pichani aliyevalia tisheti ya njano) ametueleza kwamba bomu hilo lilirushwa na kijana mmoja ambaye kimwonekano alikuwa nikijana wa miaka 20-25. alizidi kueleza kwamba baada ya kijana huyo kurusha bomu alikimbia huku akiita MWIZI MWIZI MWIZI..

KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA..
Kwabahati nzuri tulipata maelezo kutoka kwakijana ambaye alishirikiana na wananchi wengine kumkimbiza mtuhumiwa kutoka olasiti hadi katika kijiji kiitwacho ndorobo.. kijana huyo(mtizame mwisho kabisa katika post hii) alizidi kutueleza ya kuwa mtuhumiwa alikimbia kisha alijilaza katika miwa ila walisaidia na mbwa waliokuwa wakimkimbiza mtuhumiwa huyo.. mara baada ya kumkamata walimkuta akiwa na mfuko wenye bomu zilizobakia.. dakika chache wananchi wenye hasira kali walifika eneo alipokamatiwa mtuhumiwa huyo wakiwa na silaha kali za jadi wakitaka kumuua kijana huyo ndipo polisi waliokuwa wakisaidia na wananchi hao walifika eneo lile nakumchukua mtuhumiwa huyo.. 

Waaliojeruhiwa ni pamoja
na Consensia Mbaga(53) Christopher
Raymond (10),Deborah Joachim(24)
Elizabeth Isdori(24),Anna Didas(52),
Bertha Cosinery(49),Edda Ndowo(77)
,Derick Cyprian(8),Faustine Andrea
(35),Mary okech,Neema Daud(13).
Watu wengine ni Mesoit Siriri (33)
,Clenes pius(22),Joyce yohana (15)
,Restuta Alex(50), Mathias Riha (74),
Magreth Andrew(45), James Gabriel
(16), Regina James (17), Elizabeth
Masawe(15), Elizabeth Sauli(18), Njau
(35),Yasinta Msafiri (160 na Doreen
Pancras(28). Idadi wajeruhi wengine
ni Alex Arnold,Agripina Alex(9),James
Gabriel(16),loveness nelson (17)
,Amalone Pius(25),Frank Donatus (10)
,Alphonce Nyalandu (26),Athanasia
Reginald (14),Phillemon Ceressa(49)
,Neema Daud(13)Sophia Kanda(72)
,Theofrida Inocent(21), na Regina
Darnes(17).

 Picha ya kanisa hilo baada  ya mlipuko..


mmoja wa majeruhi akipatiwa huduma


 dakika chache baada ya mlipukohivi ndivyo watu walivyodhurika 
sehemu bomu lilipotua


 HUU NIMKUSANYIKO WA WATU WALIOFIKA KATIKA HOSPITALI YA MKOA YA MOUNT MERU..
 MMOJA WA MASHUHUDA AKIELEZEA JINSI MLIPUKO ULIVYOTOKEA
 VITANDA VYA KULAZIA WAGONJWA VILIZIDIWA NA KUPELEKEA KULAZA MAJERUHI WAWILIWAWILI HIVYO WASAMARIA WEMA WALIJITOLEA MAGODORO ILI MAJERUHI WAWEZE KULAZWA.

 SAMAHANI SANA KWA PICHA HII:
Hiyo ndiyo iliyokuwa maiti pekee iliyothibitika na ilishindwa kuhifadhiwa kwani haikutambulika.. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.
HUYU NIMMOJA KATI YA VIJANA WACHACHE KABISA NINAOWEZA KUTHUBUTU KUSEMA NIKIJANA SHUPAVU ALIYEWEZA KUMKIMBIZA MTUHUMIWA NA KUMKAMATA AKISHIRIKIANA NA WANANCHI NA POLISI..
hapa niakielezea tukio zima lilivyotokea na jinsi walivyomkamata mtuhumiwa