Header Ads

test

UINGEREZA YASTISHA MISAADA RWANDA

Uingereza yasitisha misaada Rwanda
Uingereza imetangaza kusitisha misaada kwa nchi ya Rwanda.
Taarifa iliyotolewa na Serikali ya Uingereza leo, imebainisha kuwa Rwanda inahusika kwa namna moja au nyingine katika mgogoro wa kivita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).


Serikali ya Uingereza imesema kuwa nchi yake haiwezi kuipa msaada Rwanda wakati yenyewe inahusika na matatizo ya kivita nchini DRC.
Imeeleza kuwa misaada ambayo ilikuwa itolewe hivi karibuni na Serikali ya Uingereza kwenda Rwanda, imesitishwa na haitatoka mingine kwa kipindi hiki.
Imezidi kubainisha kwamba endapo Rwanda itajirekebisha na kuacha kuwasaidia waasi, basi Uingereza itafikiria kurudisha misaada kwa nchi hiyo.
Uingereza imesisitiza kwamba imeamua kuinyima msaada Rwanda baada ya kupatikana kwa ushahidi usio na shaka kwamba nchi hiyo inakiwezesha Kikundi cha M23 ambacho kinaundwa na Kabila la Banyamulenge walioamua kuasi dhidi ya Serikali ya DRC.
Kabila la Banyamulenge linaundwa na Wakongo wenye asili ya Rwanda.

BY DEIWAKA