Header Ads

test

KATIKA MAKALA: ITAMBUE HISTORIA YA MAISHA YA DR SLAA.

 Huu ni mfululizo wa Makala zetu ambazo tumekuwa tukiwaletea na sasa tumeingia katika kuwa letea makala ya watu mashuhuri kuanzia Nchi,Barani Afrika na Duniani kwa ujumla.
Leo katika makala yetu tutamzungumzia Mwanasiasa Mkubwa mwenye  Heshima Nchi Tanzania na
Ulimwenguni kwa ujumla anayeipeperusha vyema bendera ya CHADEMA.


 Kwa majina kamili anaitwa WILBOARD PETER SLAA alizaliwa mwaka 29 October 1948 katika familia ya Bwana na Bibi Peter mama yake anaitwa Amelia.
Dr Slaa alianza elimu yake ya msingi katika shule ya KWERMUSI katika wilaya ya Mbulu kwa kipindi cha mwaka 1958 hadi 1961 kisha aliingia katika shule ya msingi ya Karatu iliyokuwa na darasa la 5 hadi darasa la  8 alisoma hapo kuanzia mwaka 1962hadi 1965. Baadaya kumaliza elimu ya Darasa la nane matokeo yalipotoka alikuwa nimmoja kati ya wanafunzi waliofaulu na kuwea kuchaguliwa kujiunga na Shule ya sekondari lakini ilivyotofauti na wengine yeye alijiunga na seminari ya dhehebu la Katoliki Ya Dung'unyi kwa ajili ya masomo ya sekondari ya kidato cha kwanza hadi cha nne na kuwezakumalizia elimu yake ya kidato cha sita katika seminari ya Itaga.
Baada ya kumaliza elimu ya kidato cha sita alijiunga na seminari ya Kibosho kusomea somo la falsafa bbada ya kuhitimu masomo yake hayo alijiunga tena katika seminari ya kuu ya kipalapala ambayo inahadhi ya chuo kikuu akiwa huko alijifunza somo la Theolojia. Theolojia nisomo linalohusu uhusiano wa Mungu na Binadamu. Kupitia somo hilo aliweza kujifunza Biblia, Quran Tukufu na Misahafu Mingine. Nyota ya Dr Slaa Hasa upande wa uongozi ilianzia katika chuohiki kwani alipokuwa mwaka wa mwisho aliweza kuchaguliwa kuwa Rais wa wanafunzi wa Chuo hicho.
Mwaka 1977 Dr Slaa alifanikiwa kupata upadirisho, Aliamua kujiendeleza kimasomo kwa kujiunga katika chuo kikuu cha Ponfical Urban Cha Roma cha huko Italia kisha alikwenda ujerumani kusomea stashahada katika elimu ya Jamii na Siasa.
Vyuo Vingine alivyoweza kupitia ni pamoja na St. Aquinas cha Roma alipojipatia stashahada ya Maendeleo Vijijini, Pia alipitia katika chuo cha TransWorld cha London ambapo alisomea shahada katika misingi ya Uongozi. shahada yake ya Udaktari au uzamivu katika sheria za kanisa.
Dr slaa ameandika makala mabalimbali katika magazeti na majarida.. Baadhi ya vitabu alivyoandika nipamoja na "Utimilifu Wa Msichana" na "utimilifu wa mvulana"
Mwaka 1977 Dr Slaa alianza kazi ya upadri katika jimbo la la kanisa katoliki la mbulu. Kama ilivyokawaida ya Nyota yake ya Uongozi alifanikiwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Maendeleo wa Jimbo. Mwaka 1982 Aliteuliwa kuwa msaidizi wa askofu wa jimbo la Mbulu iliyompelekea kuchaguliwa kuwa Katibu wa Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania kuanzia mwaka 1986 hadi 1991.
Baada ya kutoka kwenye upadri aliamu kuitumikia jamii yake ya Kitanzania kwa kuajiriwa  katika chama cha wasioona Tanzania akishika nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji kuanzia 1991 hadi 1995.
SIASA NA UONGOZI.
Mwaka 1980-1981 alikuwa Katibu wa Shina la CCM kwenye tawi la wizara ya mambo ya Nje jijini Roma.
Mwaka 1995 ujumbe wa wazee wa Karatu ulimtembelea Dr Slaa Na kumueleza matatizo mbalimbali Na kumuomba kugombea ubunge wa Karatu. Ambapo alijitosa mojakwamoja kupitia tiketi ya CCM. Kura za maoni zilipopigwa aliibuka na ushindi mkubwa lakini katika hali iliyowashangaza wengi jina lake lilienguliwa katika vikao vyajuu ya CCM bila sababu zozote maalum. Lakini Dr Mwenyewe alisema kuwa aliondolewa kwakuwa alikuwa sio mwenzao. lakini Ndoto yake hakutaka iishie hapo kwani alikuwa na mzigo mzito aliokuwa amekabidhiwa ya kuhakikisha anaiokoa karatu na hivyo kubadilisha mawazo na kuamua kujiunga na CHADEMA akiamini huko atapata haki. Nakweli Kwakuwa alikuwa mtu wa watu na wengi walimkubali aliweza kumbwaga mpinzani wake wa CCM kwakishindo na kufanikiwa kuwa Mbunge wa Karatu kupitia CHADEMA ambapo alianza mwaka 1995 hadi 2000.
MKOMBOZI WA WANANCHI WA KARATU.
Tatizo kubwa lililokuwa likiwasumbua WanaKaratu lilikuwa nitatizo kutu la ukosefu wa Maji lakini alipoapishwa kuwa Mbunge wa Karatu aliweza kutatua tatizo hili ambapo alishirikiana na taasisi mbalimbali za nje na Kanisa katoliki kuhakikisha Wananchi wake wanapata maji safi na Salama. Licha ya kufanikiwa kwahilo Dr aliweza kukutana na Vikwazo mbalimbali katika kutekeleza mradi huu lakini mwaka 2000 alifanikiwa.
Upande wa afya Wilaya ya Karatu ilifanikiwa kusonga mbele chini ya Dr slaa ambaye alipopata ubunge wa karatu Nivijiji 8 ndivyo vilivyokuwa na zahanati katika muda wake wa uongozi alifanikiwa kuvipatia vijiji 41 zahanati kati ya vijiji 46 vya Karatu. Pia kupitia juhudi zake Hospitali ya kanisa la kilutherani iliingia ubia na serikali na kuiwezesha hospitali hiyo kuwa hospitali teule ya wilaya.
Upande wa elimu Dr slaa Kupitia Chadema aliwezakuwahimiza wananchi kujenga shule za kata na kuboresha shule zingine zilizokuwa katika hali isiyoridhisha. Pia Kupitia ufanisi wake wa Kiutendaji amefanikiwa kuhakikisha kila kata ina shule ya sekondari na zingine za kuanzia kidato cha tano hadi sita, Na ujenzi wa Chuo Kikuu cha Karatu nao upo mbioni.
Katika kipindi chake chauongozi Karatu alifanikiwa kupunguza kodi mbalimbali ikiwamoile ya mifugo ambayo mwanzoni ilikuwa ni Tsh 500 akashusha hadi Tsh 100, Ilipunguza kodi ya kichwa kutoka Tsh 5000 hadi Tsh 2500 mwanamchi alitakiwa kulipa 500 zaidi kama mchango maalum wa mfuko wa maendeleo ya elimu kwa watoto ambao wazazi wao hawajiwezi.Halmashauri pia ilibuni vyanzovingine vya kodi. YakoMengi ambayo aliyafanya Dr Slaa alipokuwa Mbunge wilayani Karatu ikiwa nipamoja na kuendeleza miundo mbinu ya mji wa Karatu,Matengenezo ya Barabara,Kurekebisha mifereji ya maji,kuongeza upimaji wa viwanja mjini na mengine mengi..
SIFA ZAKE ZINGINE ZA UONGOZI NJE NA NDANI YA BUNGE.
1.Sifa ya kwanza nikusifika  kwa kuhudhuria vikao vya bunge pasipo kukosa labda kama kulikuwa na tatizo la msingi.
2.Ushiriki wake katika mijadala na kuuliza maswali Bungeni.
3.Kufanya utafiti hii nimmoja ya sifa amabayo ilimfanya Dr Slaa aheshimike Bungeni na kusikilizwa na wabunge wote na wananchi kwa ujumla kutokana na uwezo wake wa kulifanyia utafiti jambo analotaka kulizungumzia na kuambatanisha na ushahidi. Utafiti huu ulimsaidia kuweza kuibua mambo mbalimbali ambayo yalikuwa nyeti na kuyaweka hadharani. Ziko sifa mbalimbali alizokuwa nazo hasa katika kipindi chake cha ubunge ndani ya Bunge la Tanzania ikiwamo uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja kwa mpangilio, lingine ni tabia yake ya kuunga mkono hoja za wabunge wote alizokuwa anaona zinausahihi pasipo kuchagua chama.
Sifa nyingine kubwa ni Moyo alionao juu ya kuwa wanyonge wote kwamfano alipinga wazi kitendo cha wabunge kutaka kujiongezea mishahara kwa kiwango kikubwa na marupu wakati maelfu ya wafanyakazi wanapita katika kipindi kigumu kiuchumi pia alipinga ununuaji wa magari ya gharama yatumiayomafuta mengi kwa ajili ya wabunge na maofisa waandamizi wa serikali ilihali nayeye alikuwa ni Mbunge kitu ambacho wananchi wengi walijua labda atafurahia lakini yeye aliungana na Watanzania wote kupinga mambo hayo.
Sifa ambayo haiwezi kujificha nikupiga vita rushwa  amabapo aliziweka kashfa nyingi hadharani ikiwemo ufujaji wa pesa Benki kuu Ya Tanzania (B.O.T) , Kupitia mfuko wa madeni ya nje EPA, kashfa za Alex stewart, Mwananchi Gold na Deep Green Finance pia alishirikiana na viongozi wengine kuibua kashfa nyingi za kifisadi ikiwemo ile ya Richmond.
Pia alifanikiwa kuchaguliwa katika kamati mbalimbali za ndani na nje ya Bunge.

KUGOMBEA URAIS
Nidhahiri kuwa kutokana na ufanisi wake aliouonesha alipokuwa Mbunge ndio uliopelekea kuamini na viongozi wengine wa CHADEMA pamoja na wanachama wa CHADEMA na hivyo kumpa nafasi ya Kuipeperusha Bendera ya chama chao katika kampeni za urais.
Mwaka 2004 alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa CHADEMA nahivyokuwa mtendaji mkuu wa chama iliyopelekea kuimarika kwa chama,kupata wanachama wengi, Kuimarika kwa uhusiano wa CHADEMA na taasisi za ndani na nje ya nchi na kuimarika kwa uongozi wa CHADEMA.
Kama nilivyosema hapo awali katika kipengele hiki ufanisi wa Dr slaa ndio uliopelekea Watafiti ambao ni wasomi wa CHADEMA waliwezakufanya utafiti kwa kufuata katiba ya chama na waligundua mtu pekee ambaye angeweza kugombea urais kwa mwaka 2010 nahivyo kulipendekeza jina lake ambalo lilienda moja kwa moja katika kamati kuu ya chama na kujadiliwa,Baada ya majadiliano alionekana anafaa na kupewa nafasi hiyo.
Na bado ameaminiwa na chama pamoja na wanachama kwakumpatia nafasi nyingine ya kugombea uraisi kwa mwaka 2015.
 

DR SLAA BACKGROUND FROM PARLIAMENT OF TANZANIA
 

School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
International Eye H. Centre Certificate in Eye Health 1993 1993 CERTIFICATE
TransWorld Tutorial College, London Certificate in Management 1985 1985 CERTIFICATE
St. Thomas Aquinas University Advanced Diploma in Rural Development 1980 1981 ADV DIPLOMA
St. Urban University, Rome PhD (JCD) Law 1977 1981 PHD
Kipalapala Seminary Certificate in Theology 1974 1977 CERTIFICATE
Kibosho Seminary School Certificate in Philosophy 1972 1973 CERTIFICATE
Itaga Seminary School A-Level Education 1970 1971 HIGH SCHOOL
Dung'unyi Seminary School O-Level Education 1966 1969 SECONDARY
Karatu Primary School Primary Education 1962 1965 PRIMARY
Daudi Primary School Primary Education 1961 1961 PRIMARY
Kwermusl Primary School(Mbulu) Primary Education 1958 1960 PRIMARY
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From To
Tanzania Society for Blind Managing Director 1992 1998
Tanzania Episcopal Conference Secretary General 1985 1991
Diocese of Mbulu Development Director 1982 1985
Diocese of Mbulu Vicar General 1982 1985
Diocese of Mbulu Development Director 1977 1979
Diocese of Mbulu - Roman Catholic Church Padre 1977 1991
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
CHADEMA Secretary General 2002
CHADEMA Vice Chairman 1998 2002
CHADEMA Member of Parliament (Karatu Constituency) 1995 Todate
CHADEMA Member of National Executive Committee 1995 -
Chama Cha Mapinduzi - CCM Secretary Foreign Branch(Rome) 1980 1982
Youth Union -TANU Secretary 1974 1977
TANU Chairman (Kipalapala Branch) 1974 1977
SPECIAL SKILLS
Skill Name or Description Years Experience Acquired Through
Udiwani Course 1 -
Advanced Political Course 1 Institute for International Solidarity
Management of Eye Care 1 Centre For Eye Health, London
Special Education 1 Sight Savers International


Makala haya yamuhusuyo DR SLAA yametoka katika kitabu Kiitwacho DKT. SLAA MJENZI MAKINI WA TAIFA cha mwandishi HENRY MUHANIKA, Pamoja na vyanzo mbalimbali vya habari na kumbukumbu..






JE UNADHANI IFUATAYO ITAKUWA NIMAKALA YA MTU GANI MASHUHURI!! ILIKUWEZA KUPATA MUENDELEZO WA MAKALA YETU USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK ILIUWE UNAPOKEA HABARI NA MAKALA MOJAKWAMOJA KUPITIA FACEBOOK..